ABOUT ME

Mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu, nimebahatika kulelewa na mama na baba mlezi jijini Mbeya, kwa sasa nipo Dar aliko Baba yangu mzazi pia nafanya kazi zangu huku nikiwa naishi mwenyewe.

Nimemalizakidato cha nne mwaka 2009 na matokeo hayakuwa mazuri na kuamua kuanza kujishughulisha rasmi na kazi za Muziki na mwaka 2011 nilikuja Dar rasmi kwa ajili ya shughuli hizo.

Baada ya kufanya kazi kidogo mwaka jana (2012) nikashiriki mashindando ya vipaji vya sanaa ya muziki Epiq Bongo Star Search na Mungu akanisaidia nikawa mshindi wa mashindano hayo.

Ushindi wa EpiqBSS Umekuwa mwanzo wangu mzuri wa mafanikio katika kazi zangu za muziki na maisha kwa ujumla kwani kwa sasa nafahamika pia zawadi ya Sh. 50. Mil imenisaidia sana.

Najua sasa ni moja kati ya wasanii wa Tanzania ambapo nategemea kuendelea kufanya kazi nzuri na kukufanya wewe shabiki yangu kuendelea kuwa na mimi na kunipenda tangu umenifahamu, Nakushukuru sana na naomba tuendelee kuwa pamoja katika kazi zangu.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anisaidie nisikuangushe..

Skiliza na Download "DORO" Hapa!

Hii ndio ngoma yangu ya kwanza "SIACHI"

Ni wako Official Video