WALTER EBSS AFUNGUKA KUHUSU KUPENDWA NA UPIGAJI KURA
Mshiliki wa mashindano ya Epiq Bongo Star Search EBSS 2012/13, Walter Chilambo, ambaye pia ni mmiliki wa Blog hii, ameongelea suala la kuonyeshwa upendo na kuwa na mashabiki wengi wakati kwenye upigaji wa kura inakuwa sivyo.

Alisema kuwa isije kuwa kama kwa mshioriki mwenzake ambaye alitoka kutokana na kukosa kura za kutosha wakati anapendwa sana tu.
Walter, "Inawezekana nikawa napendwa na wengi wakitamani nishinde lakini kura zikiwa chache itashindikana kwani kura ndio kila kitu."
"Mfano mzuri ni Norman alikuwa anapendwa na wengi lakini alikuwa hapigiwi kura kitendo kilichompelekea kutoka katika mashindano"

Walter ni moja kati ya washiriki wanaowakilisha mkoa wa Dar es Salaam ingawa anatokea Mbeya kwao.
Ili kumpigia kura Walter Chilambo katika mashindano haya unaandika ujumbe mfupi (SMS) ya neno EBSS12 kwenda namba 15530.